Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFRC na UNAIDS walenga kuwatibu watu milioni 15 waishio na HIV ifikapo 2015

IFRC na UNAIDS walenga kuwatibu watu milioni 15 waishio na HIV ifikapo 2015

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu na Shirika la Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu HIV na Ukimwi, UNAIDS, yamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuendeleza juhudi za kuongeza upimaji na matibabu dhidi ya virusi vya HIV. Joshua Mmali na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOSHUA)

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, IFRC na UNAIDS zitaendelea kuchanganya utaalam na uwezo katika kuunga mkono utekelezaji wa mkataba wa UNAIDS wa kuongeza matibabu, zikilenga kuwafikia watu milioni 15 ifikapo 2015. Juhudi hizo zitahusisha kubuni mfumo wa kijamii mashinani ili kuongeza upatikanaji wa matibabu dhidi ya HIV.

Katibu Mkuu wa mfumo wa kijamii wa kuchagiza matibabu dhidi ya HIV katika IFRC, Bekele Geleta, amesema kuwa wahudumu wa afya wa kijamii mashinani wana uwezo wa kufikisha takriban asilimia 40 ya huduma zinazohusiana na HIV kwa walengwa.