Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio nchini Bahrain

Ban alaani shambulio nchini Bahrain

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la Jumatatu kwenye kijiji cha Daih nchini Bahrain kilichosababisha vifo vya polisi watatu.

Katika taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban amekaririwa akituma rambirambi kwa familia za wafiwa na kwa serikali ya Bahrain huku akisema vitendo kama hivyo haviwezi kuhalalishwa kwa sababu yoyote ile.

Katibu Mkuu amesema anaamini kwa dhati kwamba mchakato shirikishi wa kisiasa ndiyo njia pekee ya kusonga mbele. Amewataka wananchi wote wa Bahrain kuungana na kuweka mazingira bora ya kuendeleza maridhiano