Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yasambaza msaada muhimu wa chakula huko Mashariki mwa DRC

WFP yasambaza msaada muhimu wa chakula huko Mashariki mwa DRC

Shirika la Mpango wa chakula duniani, WFP limeanza kusambaza mgao wa vyakula kwa watu 74,000 walioathiriwa na mzozo wa mapigano kwenye eneo la Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Wakazi wa eneo hilo lililo mpakani mwa Uganda wamekuwa wakirejea baada ya eneo hilo kushambuliwa na kushikiliwa na waasi miezi sita ya mwisho wa mwaka jana. Kwa sasa hali ya usalama ni shwari kiasi baada ya jeshi la serikali, kurejesha utulivu na mgao wa chakula ulianza Jumanne asubuhi. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(Sauti ya Elizabeth)