Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake watakiwa kutumia mitaji midogo na uhuru kujikwamua

Wanawake watakiwa kutumia mitaji midogo na uhuru kujikwamua

Mmoja wa wanawake wafanyabiashara nchini Uganda amewasihi wanawake wenzake kutumia mitaji midogo katika kujikwamua kiuchumi na kijamii licha ya changamoto wanazokutana nazo mathalani kutopewa kipaumbele na taasisi za kifedha.

Katika mahojiano na John Kibego wa radio washirika Spice Fm ya nchini Uganda mfanyabiashara huyo Alice Kabatoro anayemiliki mgahawa na nyumba ya wageni huko Hoima, amesema licha ya baadhi ya taasisi za kifedha nchini humo kutopatia kipaumbele utoaji mikopo kwa wanawake, ni muhimu kutumia uhuru uliopo kwa wanawake sasa ikilinganishwa na miaka ya nyuma kujikwamua kiuchumi na kijamii.

(SAUTI ALICE KABATORO)