Ban ataka wavunjifu wa haki za binadamu wasifichwe

3 Machi 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehutubia kikao cha 25 Baraza la Haki za binadamu na kuelezea masikitiko kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji wa wahusika wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu, vitendo vinaavyoendelea kuzikumba nchi za Syria , Sudan Kusin na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Amesema kuwa siku zote machafuko yanaleta picha ya kusikitisha lakini masikitiko yanaongezeka zaidi pale wahusika wa vitendo vya uvunjifu wa binadamu wanaendelea kuachwa kuwa huru.Alice Kariuki na Taarifa kamili.

 (Taarifa ya Alice)

Pamoja na kuelezea masikitiko yake kutokana na vitendo vya uvunjifu wa haki ya binadamu vinavyoendelea kushika kasi katika mataifa hayo matatu, Ban alipongeza jitihada zinazochukuliwa na barazahiloza kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu duniani. Lakini pia amezilea wito nchi wanahama kutumia fursa walizonazo kuwakabili wale wote wanaohusika na vitendo vya uvunjifu huo.  Alisema watu wa namna hiyo hawapaswi kuachiwa wakiendelea kuneemeka mitaani badala yake wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

 (Sauti ya Ban)

Kwa upande mwingine amepongeza kazi kubwa inayofanywa na mashirika ya kiraia ambayo alisema kuwa yamekuwa yakijitahidi kuendeleza na kulinda haki za binadamu.

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter