Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji ya raia wasio na hatia nchini China

Ban alaani mauaji ya raia wasio na hatia nchini China

Shambulio dhidi ya raia wasio na hatia kwenye stesheni ya reli huko Kunming nchini China limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Katibu Mkuu akituma rambirambi kwa wafiwa huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Bwana Ban amesema hakuna jambo lolote linaloweza kuhalalisha mauaji ya raia wasio na hatia na amesema ni matumaini yake kuwa wahusika wa tukio hilo la Jumamosi watafikishwa mbele ya sheria.