Hali ya Ukraine yatia shaka Baraza la Usalama

28 Februari 2014

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alasiri ya leo limekuwa na kikao cha dharura na cha faragha kuhusu hali ilivyo nchini Ukraine. Kikao hicho kimefanyika kufuatia barua ya leo kwa Rais wa baraza hilo kutoka kwa mwakilishi wa kudumu wa Ukraine kwenye Umoja wa Mataifa ambapo wajumbe walipatiwa muhtasari wa hali ilivyo nchini humo kutoka kwa Naibu Msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya siasa Oscar Fernandez-Toranco.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao hicho, Rais wa Baraza hilo Balozi Raimonda Murmokaitė amesema baada ya kupokea taarifa na kufanya mashauriano wajumbe wameonyesha wasiwasi wao kuhusu kile kinachoendelea hivi sasa na wameunga mkono umoja, mamlaka na utawala wa Ukraine huku akiongeza kuwa..

(Sauti ya Balozi Raimonda)

“Baraza limekubaliana juu ya umuhimu wa pande zote za kisiasa nchini Ukraine kujizuia na kutaka kuwepo kwa mchakato shirikishi wa kisiasa unaotambua tofauti baina ya jamii mbali mbali nchini humo.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter