Elimu Tanzania yakabiliwa na changamoto

Elimu Tanzania yakabiliwa na changamoto

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kuhusu elimu kwa wote ambalo ni lengo namba mbili la Milenia, imebaini kuwa kasoro katika sekta ya elimu hugharimu serikali duniani kote dola Bilioni 129 kwa mwaka. Hii ni kwasababu asilimia 10 ya fedha zinazoelekezwa kwenye elimu ya msingi hupotelea kwenye kiwango duni cha elimu ambacho hakiwawezeshi watoto kufuta ujinga wa kutokujua kusoma.

UNESCO inasema hali hii imesababisha kijana mmoja kati ya vijana wanne kwenye nchi masikini kuwa wajinga wa kutokujua kusoma hata sentensi moja. Ripoti hiyo ambayo mwaka huu imejikita katika "Ufundishaji na kujifunza:kufikia elimu bora kwa wote" imeonya kwamba bila kuwavutia na kutoa mafunzo kwa walimu wa kutosha , mgogoro wa elimu utadumu katika vizazi na vizazi na nchi masikini ndio waathirika wakubwa Je nchini Tanzania hali ikoje? Tuungane na Penina Kajura kutoka radio washirika Afya Radio ya Mwanza Tanzania ambaye amemulika sekta hiyo.