Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

"Kili Marathon” kutumika kuepusha mimba na ndoa za utotoni

"Kili Marathon” kutumika kuepusha mimba na ndoa za utotoni

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu, UNFPA nchini Tanzania Jumapili hii itatumia mbio za kimataifa za marathoni za Kilimanjaro kueneza ujumbe wa kupinga mimba na ndoa za utotoni. Afisa wa UNFPA Sawiche Wamunza amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo kuwa hii ni mara ya pili wanadhamini mbio hizo na wanaamini ni njia muhimu ya kuwafikia vijana kwenye nchi hiyo ambayo asilimia 23 ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wamepata watoto wakiwa na umri mdogo.

(Sauti ya Sawiche)

Takwimu za demografia ya afya nchini Tanzania inaonyesha mkoa wa Shinyanga kuongoza kwa mimba za utotoni ikiwa na asilimia 59 ilhali mkoa wa Iringa una kiwango kidogo zaidi cha asilimia Nane na hali ya umaskini na ukosefu wa elimu vimetajwa kuwa kichocheo cha mimba za utotoni.

Mahojiano kamili kati na Sawiche yatapatikana kwenye tovuti yetu.