Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 140 000 kupatiwa chanjo dhidi ya Kipindupindu Sudan Kusini

Watu 140 000 kupatiwa chanjo dhidi ya Kipindupindu Sudan Kusini

Shirika la afya duniani WHO Kwa kushirikiana na serikali ya Sudan Kusini na wadau wake linaanza kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa watu wapatao 140,000 nchini humo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Chanjo hiyo ni sehemu ya akiba ya chanjo ya dharura iliyoandaliwa na WHO mwaka 2013 kwa ushirikiano wa shirika hilo na mashirika mengine ya kimataifa ikiwemo UNICEF, MSF na IFRC. WHO inasema ingawa sasa hakuna mlipuko, bado kuna hatari ya mlipuko kutokana na mazingira duni ya kiafya na watu kujazana kupindukia kwenye kambi za wakimbizi wa ndani. Chanjo hizo zitapatiwa wakazi wa kambi za Minkaman, Aweriel na kufuatiwa na Juba.Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO.

(Sauti ya Tarik)