Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukata kusababisha WFP kupunguza wigo wa operesheni zake DRC

Ukata kusababisha WFP kupunguza wigo wa operesheni zake DRC

Ukata unaoendelea kukabili shirika la mpango wa chakula duniani, WFP unalazimu lipunguze maeneo ambamo linatoa mgao wa chakula cha misaada huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Shirika hilo limesema halikadhalika litaelekeza misaada hiyo kwa wale wanaokabiliwa na uhaba mkubwa zaidi wa chakula hususan kule kulikoathiriwa na mzozo.

WFP inasema ililenga kufikia watu Milioni 4.2 kati ya Julai 2013 hadi Disemba 2015 lakini uhaba wa fedha tayari umelazimu kupinguza mgao. elizabeth Byrs ni msemaji wa shirika hilo.

(Sauti ya Byrs)