Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OPCW yakaribisha usafirishaji wa gesi kama hatua kutokomeza silaha za kemikali

OPCW yakaribisha usafirishaji wa gesi kama hatua kutokomeza silaha za kemikali

Mratibu maalum wa jopo la pamoja la Umoja wa Mataifa na OPCW kuhusu Syria Sigrid Kaag leo amekaribisha usafirishaji wa gesi ya haradali kutoka Syria kama hatua muhimu katika kutokomeza silaha za kemikali nchini humo .

Katika taarifa yake Bi. Kaag amesema jopo hilo lina matumaini ya kusafirisha bidhaa za kemikali zilizoko nchini Syria kwa njia salama, na kwa wakati unaofaa kupitia mpangilio unaotabirika na kwa viwango vya juu.

Hata hivyo linachagiza Syria kushikilia kasi ya kutekeleza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2118 na masharti ya shirika la kupinga silaha za kemikali OPCW.