Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa Ufilipino, juhudi zaidi zahitajika: OCHA

Hatua zimepigwa Ufilipino, juhudi zaidi zahitajika: OCHA

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu OCHA Valerie Amos ambaye yuko katika zaira nchini Ufilipino nchi ambayo ilikumbwa na kimbunga Typhoon Haiyan ametembelea Giana na Tacloban maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga hicho na kukiri miezi mitatau baada ya kuitembelea nchi hiyo hatua zimepigwa katika kusaidia jamii zilizoathirika.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amesema hata hivyo Bi Amos ametoa angalizo kwamba hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa.

Mkuu huyo wa OCHA ametaka wahisani kuendelea kusaidia misaada aya dharura na ile ya mpango wa muda mrefu na juhudi za maendeleo nchini Ufilipino.

Takribani kiasi cha dola milioni 400 zimechangwa kufuatia ahadi za wadau mbalimbali ili kunusuru nchi hiyo iliyoathiriwa katika Nyanja mbalimbali na kimbunga Typhoon Haiyan.