Watibuaji wa amani Yemen sasa kukumbwa na vikwazo: Azimio

26 Februari 2014

Hatua zijazo kuhusu mchakato wa kisiasa nchini Yemen zimepatiwa chepuo hii baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio kuhusu nchi hiyo likichukua hatua dhidi ya yeyote atakayekwamisha amani, usalama na utulivu wa nchi hiyo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Suala la Yemen lilikuwa ajenda ya kwanza kwenye kikao cha leo cha baraza hilo ambapo Rais wa baraza balozi Raimonda Momakaite akaweka mezani rasimu ya azimio nambari 2140 na kutaka kupigiwa kura..

Nats..

Rais anatangaza kuwa azimio limepitishwa kwa kauli moja…… . Wajumbe wakachangia wakisema ni ujumbe dhahiri kuwa Umoja wa Mataifa uko na mshikamano na matakwa na wananchi wa Yemen. Azimio mathalani linaanzisha kamati ya kusimamia uwekaji vikwazo dhidi ya watu au taasisi wanaotishia amani, ulinzi na usalama na pia linatambua kumalizika kongamano la mjadala wa kitaifa kuhusu mustakhbali wa nchi. Mwakilishi wa kudumu wa Uignereza Balozi Mark Lyall Grant akaweka bayana mchakato wa kisiasa kwa mujibu wa azimio.

(Sauti ya balozi Grant)

“Haya ni marekebisho ya uchaguzi ya kikatiba yakifuatiwa na uchaguzi. Majimbo yote yanapaswa kushirikiana kutekeleza mapendekezo ya mjadala wa kitaif. Hii yajumuisha ripoti ya utawala bora kuhusu ni nani anaweza kushika madaraka ya juu kabisa ya uongozi.”

Mwakilishi wa Yemen kwenye umoja wa Mataifa balozi Jamal Abdullah al-Salla akasema azimio la leo ni la kihistoria lakini bado kuna changamoto za matukio ya kigaidi yanayofanywa na Al Qaeda hivyo usaidizi zaidi unahitajika.

Baraza pia linajadili masuala ya Mali na Guinea-Bissau ambako uchaguzi unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.