Mradi wa kiwanda cha maziwa eneo la wafugaji laboresha maisha

26 Februari 2014

Mradi wa viwanda vya kutengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa hususan kwenye maeneo ya wafugaji nchini Tanzania umekuwa na manufaa katika kuboresha maisha ya jamii na kuwezesha kaya kukidhi mahitaji muhimu ikiwemo lishe bora na hata elimu kwa watoto wao.

Umoja wa Mataifa kupitia kituo chake cha habari nchini humo kilipata taarifa hizo wakati wa mahojiano na Schola Robert, mmoja wa wanawake wa jamii ya wafugaji mkoani Arusha aliyepata stadi na sasa ni meneja mzalishaji wa kiwanda cha Engitenterrat. Amesema wananunua maziwa kutoka kwa wafugaji na hutengeneza bidhaa kama vile jibini, maziwa ya kawaida na mtindi yanayoweza kuhifadhiwa uda mrefu

(Sauti ya Schola)