Ban alaani mauaji ya wanachuo Nigeria

26 Februari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa  mamia ya wanafunzi huko Yobe nchini Nigeria.

Wanafunzi hao waliokuwa katika chuo cha Buni Yadi kilichoko Kaskazini wa Nigeria waliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kupitia msemaji wake, Ban ameeleza namna alivyosikitishwa na mauwaji hayo na amesema kuwa anamini wahusika wake watafikishwa kwenye mkono wa dola kukabili mashtaka.

Amesema pia anaingiw ana wasiwasi namna matukio ya jinsi hiyo yanavyoendelea kushika kasi nchini humo.