Sheria ya kupinga ushoga nchini Uganda ni majanga makubwa- Global Fund

26 Februari 2014

Mpango wa kimataifa unaojulikana kama Global Fund umelaumu hatua ya kusainiwa kwa sheria inayowabinya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda na kusema kuwa hatua hiyo inazisha mashaka makubwa.

Rais wa Uganda Yoweri Mseveni hapo jana alisaini rasmi sheria hiyo ambayo inatoa kifungu cha hadi miaka 7 kwa mtu atayebainika kushiriki vitendo vya ushoga.

Sheria hiyo pia inatamka juu ya kifungo cha maisha jela kwa mhusika iwapo atarejea tena vitendo vya ushoga baada ya kuadhibiwa kwa mara ya kwanza.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanasema kuwa watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanakabiliwa na matukio ya adha kama vile vitendo vya unyanyapaa, kukosa fursa za huduma za kiafya na kutengwa na jamii.

Global Fund ambayo hutoa mafungu ya fedha kwa ajili ya kusaidia miradi ya UKIMWI  imesema kuwa kusainiwa kwa sheria hiyo ni msiba mkubwa kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter