Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru yaonekana mchakato wa amani Mashariki ya Kati: Feltman

Nuru yaonekana mchakato wa amani Mashariki ya Kati: Feltman

Kuna matumaini makubwa kwa mchakato wa amani huko Mashariki ya Kati, amesema Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Masuala ya kisiasa ndani ya Umoja huo Jeffrey Feltman alipolihutubia baraza la usalama siku ya Jumanne.

Amesema jitihada za miezi saba iliyopita za kupatia suluhu mzozo kati ya Palestina na Israeli kwa minajili ya kuwa na mataifa mawili yanaoishi sambamba zinaonekana kuwa na matunda na hivyo kudhihirisha dalili ya kupatia suluhu la kudumu mzozo huo na kuleta amani kwenye ukanda husika.

Bwana Feltman amesema ni kwa maslahi ya watu wote na hali kadhalika waisraeli na wapalestina kuwekeza ili kunufaika na hali ya sasa na kuhakikisha ina kuwa ni wa halali na manufaa kwa pande zote.

Jitihada za karibuni ni pamoja na zile za Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry za kushughulikia mzozo kati ya pande hizo kwa mizania sawa na kwa kuzingatia matarajio ya pande zote.