Ban atumai Uganda kuangalia upya sheria inayopinga ushoga

25 Februari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Mwakilishi wa kudumu wa Uganda kwenye Umoja huo Dokta Richard Nduhuura ambapo amesisitiza kuwa kila binadamu ana haki ya kufurahia haki za msingi za maisha na utu bila kubaguliwa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema Bwana Ban ameonyesha wasiwasi mkubwa kwa kusainiwa kwa sheria hiyo siku ya Jumatanu akisema suala la mtu kuishi bila ubaguzi ni mojawapo ya misingi iliyoanzisha Umoja huo.

(Sauti ya Martin)

Bwana Ban amekaririwa akiishi Uganda kulinda raia wake wote dhidi ya ghasia, ubaguzi na ameonyesha utayari wa Umoja wa Mataifa kusaidia Uganda kwenye mashauriano thabiti juu kufanikisha suala hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter