Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yasikitishwa kuendelea kwa mapiganoLibya

UNSMIL yasikitishwa kuendelea kwa mapiganoLibya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSIMIL umeelezea kusikitishwa kwake na kuendelea kwa ghasia ikiwamo mauaji, mashambulizi ya mabomu, utekwaji na mashambulizi mengine mashariki na sehemu nyingine za nchi.

Taarifa ya UNSMIL iliyotolewa leo jumanne inasema ghasia hizo zinawalenga majaji, maafisa usalama, wanaharakati, raia wakiwamo wa Kiarabu na mataifa mengine pamoja na vituo vya kupigia kura. Pia taarifa hiyo inasema mashambulizi hayo yanaelekezwa kwenye majengo ya serikali na ya kidiplomasia.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa Libya umetaka vikosi vya usalama na maafisa husika kufanya kila wawezalo kukomesha vitendo hivyo vinavyohatarisha amani nchini humo ikiwa ni pamoja na kuhatarisah usalama wa raia . Pia UNSMIL imesema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na utu na kushusha thamani ya Walibya  wakati huu ambapo Libya iko katika shauku ya kujenga taifa lenye msingi wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.