Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM yabainisha umuhimu wa ushirikiano kwa nchi za Uarabuni

Ripoti ya UM yabainisha umuhimu wa ushirikiano kwa nchi za Uarabuni

Imeelezwa kuwa nchi za kiarabu zitakuwa na mafanikio makubwa ikiwa zitashirikiana katika maswala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, imesema ripoti ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa ajili ya nchi za Asia Magharibi ESCWA.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa leo hukoTunisiana Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dokta. Rima Khalaf imebainisha maono ya uwiano kama kiungo muhimu kwa maendeleo katika eneohilo

Mmoja wa waandishi wake Abdallah Al Ardari ambaye ni mchumi Mkuu katika ESCWA anasema kwamba uwiano unapaswa kupimwa.

Ameongeza kwamba kile wanapendekeza ni mpango na hatua ambazo zinaweza kutekelezwa ndani ya hali halisi ya kisiasa iliyopo katika eneohilo.

Hatua za kwanza amabazo zitawezesha uwiano wa kiuchumi zitajumuisha kupunguza gharama za usafiri baina ya nchi za kiarabu, kulegeza vizuizi vya kazi na kupunguza ushuru wa biashara