Janga la kibinadamu Syria laangaziwa ndani ya Baraza Kuu la UM

25 Februari 2014

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria wakati huu ambapo janga lililokumba nchi hiyo likiingia mwaka wa nne. Flora Nducha na Ripoti kamili.

(Ripoti ya Flora)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na viongozi wengine waandamizi wa mashirika ya umoja huo ikiwemo UNHCR, WHO, OCHA na haki za binadamu walihutubia mjadala huo kwa kiasi kikubwa wakirejelea kauli zao kuwa janga la kibinadamu nchini Syria sasa yatosha.

Wamesema huduma za kijamii zimeporomokakamavile elimu, na hata hospitali zimegeuzwa hifadhi ya watu wenye silaha, na huduma hazifikii walengwa. Bwana Ban amesema anafuatilia utekelezaji wa azimio la baraza la usalama kuhusu hali ya kibinadamu na anatakiwa atoe ripoti ndani ya siku thelathini, hivyo akasema ..

(Sauti ya Ban)

"Kuzuia kufikia watu wenye mahitaji ya dharura ya chakula maji au vifaa tiba ni ukiuikwaji wa msingi wa haki zao za uhai na utu, na bado kuna ripoti za mauaji na kushikiliwa, mauaji na mateso. Jamii ya kimataiaf inaendelea kufuatilia haki na uwajibikaji kwa ukiukwaji wa haki.”

Kamishna Mkuu wa UNHCR, Antonio Gutteres akaenda mbali zaidi..

(Sauti ya Gutteres)

"Na ijapokuwa wakimbizi wameweza kupata makazi kwa kuvuka mpaka na kuingia nchi jirani, bado hawawezi kukukwepa msongo wa akili kutokana na walichoshuhudia. Mtoto Alfa aliye Lebanon hajaweza kuzungumza kwa miezi 12 tangu ashuhudie baba yake akiuawa na nyumba yao ikiteketezwa huko Syria.”

Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay akasema pande zoteSyriazinashindwa kufahamu kuwa hakuna suluhu la kijeshi nchini humo akisema watoa huduma za binadamu wanakumbwa na madhila ikiwemo mashambulizi  ya dhahiri pindi wanapojitoa kuhudumia majeruhi.

Amerejelea wito wake wa kutaka suala laSyrialiwasilishwe mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter