Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapiamlo kitisho kinachoibukia miongoni mwa wakimbizi wa Syria: UNICEF

Utapiamlo kitisho kinachoibukia miongoni mwa wakimbizi wa Syria: UNICEF

Tathmini ya pamoja ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake kuhusu hali ya wakimbizi wa Syria nchini Lebanon imezindulia leo na kufichua utapiamlo kama mojawapo ya kitisho kinachoibukia. Mathalani kwenye bonde la Bekka na maeneo ya kaskazini mwa Lebanon visa vya utapiamlo uliopindukia miongoni mwa wakimbizi vimeongezeka maradufu mwaka 2013 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Nchini Syria takribani watoto 2,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano wako hatarini kufariki dunia kutokana utapiamlo iwapo hawatapatiwa tiba. Patrick McCormick ni msemaji wa UNICEF.

(Sauti ya Patrick)