Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna uwezekano wa raia kushambuliwa huko CAR: UNHCR

Kuna uwezekano wa raia kushambuliwa huko CAR: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeonya kuwa takribani raia 15,000 wamezingira na vikundi vilivyojihami huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuna hatari ya kwamba wanaweza kushambuliwa wakati wowote. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Idadi kubwa ya walionaswa kwenye mazingira hayo ni waislamu walioenea katika maeneo 18 kaskazini-magharibi na kusini-magharibi mwa nchi pamoja na baaadhi ya viunga vya mji mkuu Bangui.

UNHCR inasema wanamgambo hususan kutoka kikundi chenye wakristu wengi cha Anti-Balaka wanatishia kushambulia na hivyo shirika hilo linaomba jeshi la kimataifa lililopo Jamhuri ya AFrika ya Kati kutoa usaidizi wa ulinzi. Adrian Edwards ni msemaji wa shirika hilo.

(SAuti ya Adrian)

UNHCR na wadau wetu tunashughulikia hali hii kupitia ulinzi..kwa kuwepo au kutoa usaidizi wa kibinadamu na utetezi wa ulinzi wao na katika mazingira ya kipekee kuwezesha jamii kuhamia maeneo salama. Lakini jitihada hizi pekee haziwezi kuwa suluhu ya mzozo huu. Tunasihi tena vikundi vyote vyenye kujihami viache mashmbulizi ya jumla dhidi ya raia. Tunaomba vikosi zaidi vipelekwe nchini humo kwani idadi yao ni ndogo sasa kulingana na ukubwa wa nchi katika kushughulikia mzozo uliopo. Serikali inahitaji msaada zaidi kwa kuongezewa polisi na kuundwa upya kwa mfumo wa mahakama ili kumaliza ukwepaji sheria. Vikundi vilivyojihami vyapaswa kupokonywa silaha na kujumuishwa katika jamii iwapo itawezekana."