Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay asikitishwa na Uganda kupitisha sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja

Pillay asikitishwa na Uganda kupitisha sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja

Saa chache baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutia saini na kuwa sheria muswada unaopinga mapenzi ya jinsia mmoja, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameeleza kusikitishwa na hatua hiyo akisema ni matumaini  yake kuwa itafanyiwa mapitio haraka iwezekanavyo ili kulinda haki za binadamu za kundi hilo.

Katika taarifa yake Bi. Pillay amesema sheria hiyo inayoharamisha ushoga na hata waliobadili jinsi zao ni kinyume na haki za binadamu kwani wahusika wa vitendo hivyo nchiniUgandasasa watakabiliwa na adhabu ikiwemo kifungo cha maisha na adhabu kwa watetezi wao.

Amesema kupinga ushoga na mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watu hakuhalalishi kuvunjwa kwa haki ya binadamu kwa wengine na hivyo Pillay amesema serikali yaUgandaina wajibu kupitia katiba yake na sheria za kimataifa kuheshimu haki za binadamu za watu wote na kuwalinda dhidi ya ubaguzi na ghasia.

Halikadhalika amesema kupitishwa kwa sheria hiyo ni pigo kwa harakati za kupambana na Ukimwi kwani mara nyingi kundihilohukumbwa na ubaguzi kwenye upataji wa tiba na hata taarifa kuhusu ugonjwa huo.