Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka wa kimataifa wa visiwa vidogo wazinduliwa rasmi

Mwaka wa kimataifa wa visiwa vidogo wazinduliwa rasmi

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limezindua rasmi mwaka wa kimataifa wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea, SIDS kwa lengo la kuangazia changamoto na fursa katika maeneo hayo hususan wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

(Taarifa ya Alice)

Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa moja ya changamoto kubwa kaw nchi za visiwa vidogo zimeendelea na hivyo kushindwa kusongesha uchumi wao, amesema Rais wa Baraza Kuu John Ashe wakati wa uzinduzi wa mwaka huo mjini New York. Amesema mazingira ya kuvutia ni bora kwa watalii lakini bado vipato vyake vinashindwa kukwamua maisha ya wananchi wao.

(Sauti ya Ashe)

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema baraza kuu halijawahi kutenga mwaka maalum wa kundi la nchi lakini hatua hii ni ya kipekee hivyo…

(Sauti ya Ban)

Nchi za visiwa vidogo zinazoendelea ni pamoja na Seychelles, Cuba, Mauritius na Jamaica.