Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Museveni atia saini sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja

Rais Museveni atia saini sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja

Hatimaye  Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ametia saini sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja huku Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu Navi Pillay akieleza masikitiko yake na hatua hiyo akisema kuwa ni matumaini yake itapitiwa upya mapema iwezekanavyo ili kulinda haki za binadamu za kundihilo. John Kibego wa Radio washirika Spice FM Uganda na ripoti kamili.

(Tarifa ya John Kibego)

Kwa sasa yeyote atakayepatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwa zaidi ya mara moja, atakabidhiwa kifungo cha maisha jela. Adhabu hiyo pya inawapata wale wanaohushisha watoto, watu wenye ulemavu na wale waliowambukiza virusi vya ukimwi. Kwa Yule atakayepatikana na hatia hiyo kwa mara ya kwanza atakabidhiwa kifungo cha miaka 14. Mara baada ya kutia saini mswada huo rais Museveni amesema Uganda inaweza siimaama bila msaada badala ya kukubali mapenzi hayo.

(Sauti ya Raisi Yoweri Museveni)

“Wageni hawawezi tulazimisha cha kufanya. Hii ni nnchi yetu, ni jamii yetu, ni mustakabali wetu si mustakabali wa mtu muingine. Ikiwa hawapendi kutupa misaada, waache. Uganda ni nchi tajiri hatuhitaji misaada. Kiukueli misaada ni sehemu ya tatizo”

Wananchi wengi wamefurahia sheria hii kwa kutunza mila na desturi lakini wengine hawajafurahi kwa kuhofia haki za binadamu huku wengine wakihofia matatizo ya kiuchumi baada ya nchi kama Marekani kutishai kuondoa misaaada yao juu ya sheria hii.