Ban asikitishwa na kinachoendelea nchini Thailand

24 Februari 2014

Kile kinachoendelea huko Thailand kimeripotiwa kumsikitisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akitaja zaidi mashambulio ya kutumia silaha dhidi ya raia ambayo yamesababisha kuuawa hata kwa watoto.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Katibu Mkuu akitaka ghasia hizo kusitishwa mara moja na serikali kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.

Bwana Ban amesema anaamini kwa dhati kuwa hakuna sababu ya ghasia kutoka upande wowote katika kupatia suluhu tofauti za kisiasa na mizozo. Amezisihi pande zote kuheshimu haki za binadamu na utawala wa kisheria sambamba na kuzuia mashambulio mapya.

Amezitaka pande hizo kuingia katika mashauriano ya dhati ili kumalia mzozo huo na kusongesa mbele marekebisho huku akisema yuko tayari kusaidia kwa njia yoyote ile inayowezekana.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud