Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na wananchi wa CAR kupitia Radio awasihi waweke silaha chini

Ban azungumza na wananchi wa CAR kupitia Radio awasihi waweke silaha chini

Ni sauti  ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akizungumza kwa lugha ya Sango ya huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, akikijitambulisha kwa wananchi wa nchi hiyo mwanzoni kabisa mwa  ujumbe wake maalum aliowapelekea kupitia radio.
Baada ya salamu Bwana Ban ambaye ametuma ujumbe huo pia kwa lugha ya Kifaransa na kiingereza, anawahakikishia wananchi hao walio katika zahma ya mapigano ya kwamba hawako peke yao na hivyo anasema…
(Sauti ya Ban)
“Niko hapa kueleza mshikamano wangu na usaidizi kwa wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hamko peke yenu! Mataifa mengi yanajitahidi kusaka amani! Nimeomba jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua zaidi! Askari na polisi wengi wanalinda raia, misaada zaidi kuokoa maisha. Nawasihi na ninyi, wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na upinzani, acheni mauaji. “
Katibu Mkuu akaelekeza ujumbe kwa vikundi vinavyopigana…

(Sauti ya Ban)

“Acheni mauaji. Wekeni silaha zenu chini. Wale wanaofanya ghasia wanaigawa na kuiharibu nchi yenu pendwa. Waislamu na wakristu mmejenga nchi yenu kwa pamoja. Nafahamu mtafanya hivyo tena. “
Katibu Mkuu amesema yuko pamoja na wananchi hao na amewaahidi usaidizi wake wote kwa ajili ya amani na maridhiano, haki na uwajibikaji kwa wananchi wote wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.