Baraza la Usalama lalaani shambulio la kigaidi Somalia

21 Februari 2014

Baraza la Usalama limelaani shambulio la kigaidi nchini Somalia nakusababisha vifo na majeruhi kadhaa ambapo kundi la kigaidi la Al Shabaab limekri kuhusika katika shambulio hilo lililolenga ofisi ya Rais wa taifa hilo.

Taarifa ya baraza hilo iliyotolewa mjini New York leo ijumaa imesema baraza la usalama limetuma rambarambi kwa familia za wahanga, watu na serikali ya Somalia huku pia likiwatakia uponyaji wa haraka majeruhi wa shambulio hilo.

Baraza hilo la usalama limesisitiza kuwa masgmbulizi kama hilo na mengineyo ya kigaidi halitadhoofisha nia ya kuendelea kusaidia amani na mchakato wa utengamano wa Somalia.

Pia baraza limetaka kufikishwa katika mkono wa sheriaq kwa wapangaji, wawezeshaji na watekelazaji wa shambulio hilo na kuzikumbusha nchi wajibu wao wa kuhakikisha hatua za kutokomeza ugaidi zinachukuliwa chini ya sheria ya kimataifa hususani haki za binadamu, wakimbizi na sheria ya kiutu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter