Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha makubaliano kati ya pande kinzani Ukraine

Ban akaribisha makubaliano kati ya pande kinzani Ukraine

Katibu Mlkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametiwa moyo na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais Yanukovych wa Ukraine na viongozi wa upinzani ikiwa sehemu ya mchakato wa kurejesha utulivu nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bwana Ban alimpigia simu Rais Yanukovych akielezea pongezi zake kwa hatua hiyo huku akisisitiza utekelezaji wa haraka wa makubaliano hayo ili kuepusha kuzorota zaidi kwa hali ya usalama nchini humo.

Amesifu mashauriano na ulegezaji misimamo baina ya pande husika na ushirikiano wa kimataifa wa kupatia suluhu mzozo huo.

Halikadhalika Katibu Mkuu amekaribisha kitendo cha bunge hapo jana kusaini azimio lililowezesha kuondoka kwa polisi kutoka mji mkuu Kiev.

Amesisitiza ombi lake la kuepuka vurugu na badala yake mazungumzo yabakie kuwa njia kuu ya kupatia jibu sintofahamu iliyopo.

Amesema ni matumaini yake kuwa maendeleo ya hivi karibuni yatafungua njia kwa pande husika nchini huku kusuluhisha mzozo na hatimaye kuingia katika mchakato sahihi wa marekebisho.