Lugha ya mama ina umuhimu katika kuinua kiwango cha elimu

21 Februari 2014

Februari 21 ni siku ya lugha ya mama duniani, siku hii huadhimishwa kusherehekea uwepo wa lugha nyingi na tamaduni tofauti kote ulimwenguni. Lugha ya mama ni lugha ya kwanza imtokayo mtu pale anapoanza kuwa na uwezo wa kuzungumza. Mtu anaweza kuwa ni raia wa Uganda na kabila lake ni muankole, lakini akazaliwa Marekani na iwapo lugha ya kwanza kuifahamu ni Kiingereza basi hiyo inakuwa ndiyo lugha ya mama kwake yeye.

Siku hii ilianzishwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika kuimarisha , kudumisha na kulinda lugha zote zinazotumika na watu tofauti duniani.

Maadhimisho ya mwaka huu yanalenga umuhimu wa lugha ya mama katika somo la sayansi. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la Sayansi na utamaduni Irina Bokova amesema kutenga lugha yoyote ni sawa na kuwatenga wenyeji wa lugha hio kutoka kwa haki yao ya kupata elimu.

Nchini Kenya taifa ambalo lina zaidi ya lugha 42 za mama, swala la kabila huzua hisia tofauti. Je Wakenya wanasema nini kuhusu umuhimu wa lugha ya mama? Basi ungana na Geoffrey Onditi wa Radio washirika la Shirika la utangazaji la Kenya, KBC ambaye ameongea na wakenya katika kuadhmisha siku hii.

(PCKG Geoffrey )

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud