Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko Ukraine hayakubaliki: UM

Machafuko Ukraine hayakubaliki: UM

Jopo la  wataalamu huru wa Umoja wa Matifa leo limetaka kusitishwa hima kwa machafuko mjini Kiev Ukraine ambayo yameshuhudia vifo vya raia  na vikosi vy ausalama.

Taarifa ya jopo hilo kwa vyombo vya habari inamnukuu Chaloka Beyani, anayeongoza kamati ya kuratibu wataalamu wa kimataifa iliyoteuliwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Bwana Beyani amesema jopo hilo linalaani matumizi ya nguvu za ziada kutoka kwa vikosi vya usalama dhidi ya waandamaanaji na kuongeza kuwa wanataka kuwepo kujizuia pamoja na uchunguzi wa haraka , huru na wa kina kuhusu vitendo vya vikosi vya usalama.