Wavuvi wadogowadogo kupigwa chepuo na FAO

21 Februari 2014

Huenda wavuvi wadogo wadogo wa samaki wakanufaika kutokana na shirika la chakula na kilimo FAO kuwasaidia wavuvi hao hususani katika nchi zinazoendelea hatua ambayo itawasaidia wavuvi hao kupata faida kutokana na kukua kwa soko la bidhaa hizo duniani

Katika mahojiano na Sandra Ferrari wa radio ya Umoja wa Mataifa mchambuzi wa mipango ya samaki kutoka FAO Nicole Franz, amesema wavuvi wadogo wadogo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo

SAUTI

(NICOLE FRANZ)

Kiwango cha maliasili samaki kinapungua, kwa hiyo samaki hawatoshi kuwa kitoweo kwa kila mmoja na kutoa ajira , pia kuna suala la ushindani wa rasilimali mathalani katika maeneo ya Pwani kuna maendeleao ya watalii, kilimo. Sekta hizi zinaweka shinikizo katika sekta ya wavuvi wadogo wadogo.

Nini kifanyike?

SAUTI

(NICOLE FRANZ)

"Wanachohitaji ni maazingira yatakayowawezesha kunufaika na haki walizonazo ambazo labda hawazijui au hawawezi kuzidai."

Uzalishaji wa samaki kimataifa unatarajiwa kufikia tani milioni 160 mwaka 2013 kutoka tani milioni 157 mwaka 2012.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud