Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zoezi la kuwahamisha kwa hiari wakimbizi wa Somalia walioko Kenya kuanza tena

Zoezi la kuwahamisha kwa hiari wakimbizi wa Somalia walioko Kenya kuanza tena

Zoezi la kuwarejesha makwao kwa hiari wakimbizi wa Somalia walioko nchini Kenya linatarajiwa kuanza tena baada ya mabadiliko ya serikali nchini Somalia ambayo yalisababisha kusitishwa kwa zaoezi hilo.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii msemaji wa ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi nchini Kenya Abel Mbilinyi amesema ziara ya waziri mkuu mpya wa Somalia nchini humo imefufua matumaini ya kuanza tena kwa zoezi hilo

( SAUTI MBILINYI )

Katika hatua nyingine Bwan Mbilinyi amesema UNHCR nchini Kenya inaendelea kupokea wakimbizi wa Sudani Kusini wanaosaka hifadhi nchini humo huku akisema wingi wa wakimbizi hao umeibua changamoto kadhaa ikiwamo upungufu wa ardhi na mahitaji mengine ya msingi

(SAUTI MBILINYI )