Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofauti kati ya maskini na tajiri duniani yazidi kuongezeka: Ban

Tofauti kati ya maskini na tajiri duniani yazidi kuongezeka: Ban

Viongozi waandamizi ndani ya Umoja wa Mataifa wamepaza sauti zao hii leo siku ya kimataifa ya haki ya kijamii wakitaka mamlaka kote duniani kuchukua hatua kujenga mazingira ya ustawi bora kwa wote kwani tofauti kati ya maskini na tajiri inazidi kuongezeka kila uchao.

Miongoni mwao ni Katibu Mkuu wa Ban Ki-Moon ambaye amesema tofauti hiyo si kati ya nchi na nchi tu, bali pia ndani ya nchi hata zile zenye ustawi.

Amesema mahali mtu atokako, mrengo wake wa kisiasa, jinsia yake na hata kabila lake havipaswi kubainisha kipato au fursa yake kielimu. Hivyo ametaka mshikamano wa dunia kuondokana kuweka fursa kwa wote.

Naye Rais wa Baraza Kuu John Ashe ametaka jamii ya kimataifa kutambua kuwa usawa na haki ya kijamii ni muhimsu kwa uhusiano wa kimataifa kwenye karne ya 21.