Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twakabiliwa na janga la kijamii., wanasiasa hawapaswi kupuuza : ILO

Twakabiliwa na janga la kijamii., wanasiasa hawapaswi kupuuza : ILO

Wakati dunia inaadhimisha siku ya haki ya kijamii hii leo, shirika la kazi ulimwenguni, ILO linasema hali ya kijamii si shwari kwani vijana wamekata tamaa na hakuna mwanasiasa anayeweza kuepuka kutambua hilo na hivyo ILO imetaka wanasiasa kuungana na kuwa na kauli moja juu ya kuondokana na hali hiyo. Alice Kariuki na ripoti kamili.

(Taarifa ya Alice)

Hii leo kizazi cha vijana hakifahamu majaliwa yake, hakina matumaini ya ustawi kama ilivyokuwa kwa wazazi wao na wengi wao wamekata tamaa amesema Mkurugenzi mkuu wa ILO Guy Rider kwenye ujumbe wake wa siku ya leo.

Amesema huo ndio ukweli halisi na hakuna mtunga sera yoyote anayeweza kupuuza kwani harakati za miaka sita za kujikwamua kutoka mdororo wa kiuchumi zimetumbukiza jamii kwenye hali ngumu zaidi. Ryder anahoji iwapo watunga sera wako tayari kuchukua hatua.

(Sauti ya Ryder)

"Tunapokabiliwa na janga la kijamii na janga la haki ya kijamii tunasihi kuunganisha jitihada za watunga sera na utungaji sera kwenye dira na matamanio ya ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 ya kukwamua watu wote ambayo itasaidia kuondoa wote kwenye ufukara.”

Mkuu huyo wa ILO amesema nchi kama Msumbiji, Brazili na hata Thailand zimedhihirisha hatua thabiti za kuondokoana na janga hilo licha ya mazingira magumu zinazozikabili hivyo ni mfano wa kuigwa..