Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya afya ni muhimu kuelekea kikomo cha MDGS : Balozi Mero

Sekta ya afya ni muhimu kuelekea kikomo cha MDGS : Balozi Mero

Wakati zikiwa zimesalia siku zisizozidi elfu moja kufikia kikomo cha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015 mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, balozi Modest Jonathan Mero amesema sekta ya afya inahitaji msukumo zaidi katika kutekeleza malengo hayo.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Balozi Mero ambaye hivi karibuni alikutana na Mkuu wa shirika la afya duniani Dkt. Magaret Chan, amesema anatarajia kukutana pia na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mapambano dhidi ya ukimwi katika juhudi za kujadili mbinu za kutekeleza lengohilola sita.

(SAUTI Balozi MERO)

Hata hivyo balozi Mero amesema katika mkutano w ke wa awali na mkuu wa WHO wamejadili namna wanavyoweza kushirikina katika kuimarisha sekta ya afya.