Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO  yafafanua kuhusu kuenea kwa virusi vya A(H7N9

FAO  yafafanua kuhusu kuenea kwa virusi vya A(H7N9

Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO limesema kuwa hakuna ushahidi wowote unaonyesha kwamba binadamu aliyeathiriwa na virusi vya homa ya mafua ya ndege  A(H7N9), alipata maambukizi kutoka kwa wanayama lakini kuna kiwango kidogo cha virusi kinaweza kuambukizwa kwa wanyama ikiwemo jamii ya ndege.

Taarifa hiyo ya FAO imekumbusha juu ya tukio la mtu mmoja kuathiriwa na vurusi hivyo nje ya China ambaye baadaye aligundulika huko Malaysia.Taarifa ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Alice Kariuki)

Mgonjwa huyo anayetoka katika jimbo la Guangdong nchini  China, ambako ndiko anakodhaniwa alikokubwa na maambukizi hayo, alikuwa akitembelea Malaysia  kama mtalii . Kutokana na maambukizi hayo kwa hivi sasa amelazwa hospitalini.

Jimbo la  Guangdong ni moja maeneo ambayo yanaripotiwa kuathiriwa zaidi na virusi hivyo katika kipindi cha mwaka huu 2014.

Afisa wa wanyama wa FAO Juan Lubroth amesema kuwa dunia haipaswi kushtushwa zaidi na maambukizi hayo lakini hata hivyo ameonya kuwa inapaswa kuwa makini .

Taarifa zinaelezwa kwamba baadhi ya watu walioambukizwa na virusi hivyo katika mataifa mengine kutokana na hali yao ya kukaribiaana na mifugo jamii ya kuku.