Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitikia kuzorota kwa hali ya haki za binadamu Korea Kaskazini

Ban asikitikia kuzorota kwa hali ya haki za binadamu Korea Kaskazini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa bado anaendelea kusalia katika hali ya wasiwasi mkubwa kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini Korea ya Kaskazini.

Ameeleza hali hiyo kufuatia ripoti iliyotolewa na kamishna maalumu iliyokwenda nchini humo kuchunguza juu ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu.

Ban amesema ripoti hiyo itaamsha jumuiya ya kimataifa ili ifahamu namna haki za binadamu zinavyoendewa kinyume nchini humo.

Aliitaka pia Korea kuendelea kushirikiana na jumuiya za kimataifa ili kuimarisha hali za haki za binadamu.