Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa kali yaikumba Somalia, misaada ya dharura yahitajia: UM

Njaa kali yaikumba Somalia, misaada ya dharura yahitajia: UM

Hali mbaya ya kiutu inayosababishwa na njaa nchini Somalia ni lazima itatuliwe kwa kuchangisha fedha zaidi ili kukomboa kuwa watu takribani milioni mbili ambao hawana uhakika wa chakula.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York mkuu wa opereseheni za ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA Bwana John Ging ambaye amekuwa ziarani nchini Somalia kutathimini hali ya kiutu a

mesema kudorora kwa usalama kunachangia kuongezeka kwa njaa huku pia akitaja hali ya hewa mbaya kuwa moja ya kichochezi cha hali hiyo.

(SAUTI GING)

"Wasomali wametekeseka kwa takribani miaka 25 mfululizo hatuwezi kurudui nyuma katika kazi yetu ya kuwa nao, kuwasaidia kutatua hali hii tete ambyo ipo tayari na kuendelea kuwasaidia, kujijenga upya ili wawe yatari kukabiliana na majanga katika siku za usoni."

Hata hivyo amesema amefurahishwa na namna utawala wa sasa wa Somalia unavyoonyesha nia ya kukomboa nchi kwa kuweka mbele maslahi ya watu. Amesema kiasi cha dola milioni 900 zinahitajika ili kusaidia kukwamua taifa hilo dhidi ya ukosefu wa chakula.