Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mauaji vijijini Nigeria

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mauaji vijijini Nigeria

Ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, imelaani vikali mashambulizi yalotekelezwa mnamo Jumapili na watu wenye silaha dhidi ya vijiji 8 katika majimbo ya Adamwa na Borno, nchiniNigeria, na kuwaua watu zaidi ya 150.

 Ripoti zinasema watu wapatao 65 waliuawa katika vijiji 7 kwenye jimbo la Adamwa, huku wengine 90 wakiuawa katika kijiji cha Izge kwenye jimbo la Borno.

 Wakazi wengi sasa wameyakimbia makazi na vijiji vyao kwa kuhofia mashambulizi zaidi. Ravina Shamdasani ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

 (Sauti ya Ravina)