Radio ni chombo chaa kijamii hususani Afrika: Dkt Hamza Mwamoyo

16 Februari 2014

Radio ni chombo cha habari kwa makundi yote kwa wasomi na wasio wasomi na pia chombo hiki hutumika kama chombo cha kijamii barani Afrika amesema mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya sauti ya America VOA  Dkt. Mwamoyo Hamza wakati akihojiwa an Sunday Shomari wa idhaa hiyo aliyewakilisha idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa katika kupata maoni ya mkuu wa VOA kuhusu maadhimisho ya siku ya radio Februari 13 yaliyoangazia uwezeshaji wa kijinsia kupitia radio.

 Hata hivyo amesema waandaji wa vipindi vya radio wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha vipindi wanavyoandaa vinawafanya wanawake wajumuishwe na kushiriki kwa ustawi wa kundi hilo.Hapa anaanzakwa kuelezanafasi ya radio katika upashanaji taarifa.