CITES yakaribisha azimio la London kuhusu biashara haramu ya wanyama wa pori

14 Februari 2014

Sekritariati ya Kamati ya kudhibiti biashara katika viumbe vilivyo katika hatari ya kuangamizwa, CITES, imekaribisha kaongamano la London kuhusu biashara haramu katika wanyama wa pori, ambalo lilifanyika Februari 12-13. Kongamano hilo liliandaliwa na serikali ya Uingereza na familia ya kifalme ya Uingereza, na kuleta pamoja wawakilishi wan chi 46 na mashirika 11 ya kimataifa ili kuweka utashi wa ngazi ya juu kisiasa katika juhudi za kukabiliana na uhalifu unaowahusu wanyama wa pori.

Katika kongamano hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague, alisema kuwa ni wazi kuwa kiwango cha uhalifu unaowahusu wanyama wa pori sasa ni tatizo ambalo halijawahi kushuhudiwa, akitaja mifano ya makumi ya maelfu ya tembo kuuawa mwaka ulopita, na vifaru zaidi ya 1,000 kuuawa katika uwindaji haramu. Ameongeza kuwa kuna viumbe wengine wengi ambao wamo hatarini, na kusema kuwa hili ziyo tu tatizo la kimazingira, lakini ni sekta ya uhalifu wa kimataifa, ambayo inaenda sambamba na ulanguzi wa madawa haramu, silaha na usafirishaji haramu wa watu.

Akilihutubia kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa CITES, John E. Scanlon, amesisitiza kuwa tabia za wanadamu kama vile kutoridhika, kutojua na kutojali ndivyo vitu vinavyochangia biashara haramu katika viumbe vya porini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud