Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Syria yaendelea Geneva pande kinzani zatoa masharti

Mazungumzo ya Syria yaendelea Geneva pande kinzani zatoa masharti

Awamu ya pili ya mkutano wa kusaka amani nchini Syria unaendela mjini Geneva ambapo hii leo pande zinazokinzana zimekutana na waandishi wa habari kuzungumzia hatua za mazungumzo hayo.

Msemaji wa serikali Naibu waziri wa mambo ya nje Faisal Makdad amesisitiza dhamira ya kukomesha umwagaji damu ili kufikia amani ya kweli.

Tuanataka kuendelea na majadiliano yetu mpaka tufikie makubaliano katika hatua hii kwa kuwa ni muhimu kwa ajili ya watu wa Syria, na wale wanaodai wanaiwakilisha Syria lazima waahidi kukomesha umwagaji damu Syria.

Kwa upande wake msemaji wa upinzani Louay Safi amesisitiza kuwa mapendekezo ya namna ya demokarsia ya mpito pamoja nasuluhisho la kisiasa ndiyo hatua muhimu kuelekea katika makubaliano. 

Upinzani umewasilisha mapendekezo kwa Ibradhimi na serikali juu ya namna tunavyoweza kuwa na demkrasia ya mpito na suluhisho la kisiasa mapendekezo hayo yako mezani lakini serkali bado haijawasilisha yao kuhusu mpito wa kidemokrasia, kuepuka utawala wa kiimla na kuondokana na umwagaji damu, tunasubiri kuona ikiwa serikali itajihusisha katika suluhisho la kisiasa