Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinachoendelea Venezuela kinatutia shaka: Ofisi ya haki za binadamu

Kinachoendelea Venezuela kinatutia shaka: Ofisi ya haki za binadamu

Ofisi ya Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imeelezea wasiwasi wake juu ya ongezeko la ghasia nchiniVenezuela, ikitaja zaidi tukio la vifo vya watu wapatao watatu wakati wa maandamano kwenye mji mkuu Caracas, Juzi Jumatano.

Msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville akizungumza na waandishi wa habari mjiniGeneva, Uswisi amesema maelfu ya watu kwenye miji yote mikubwa nchini humo ikiwemoCaracaswaliripotiwa kuandamana kupinga kushikiliwa kwa wanafunzi waliondamana awali pamoja na ongezeko la matukio ya uhalifu na hali ngumu ya kiuchumi.

Colville amesema tayari Mwendesha mashtaka nchini Venezuela amethibitisha vifo vya watu watatu, majeruhi 66 na watu 69 kushikiliwa kwa tuhuma za kushiriki maandamano hayo jambo ambalo amesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inataka serikali ihakikishe inazingatia haki ya uhuru wa kujieleza.

Halikadhalika imeitaka wahusika wa ghasia wafikishwe mbele ya sheria.