Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafasi ya wanahabari wanawake Kenya yaangaziwa; Yaelezwa hatua zimepigwa

Nafasi ya wanahabari wanawake Kenya yaangaziwa; Yaelezwa hatua zimepigwa

Radio ni chombo muhimu katika jamii iwe ni katika kutoa habari kuelimisha na kwa ajili ya burudani hususan katika nchi zinazoendelea. Chombo hiki ni muhimu pia katika kujenga mustakhabli wa jamii kwa ujumla. Radio hutumika katika kupigania haki katika jamii. Ijapokuwa chombo hiki kina faida nyingi ama watangazaji hususan wanawake hukumbana na changamoto nyingi wakati wa kutekeleza wajibu wao .

Ikiwa leo  Fenruary 13 ni siku ya Radio duniani kuna baadhi ya hatua ambazo zimepigwa lakini bado kuna pengo katika kuweka usawa kati ya wanahabari wa kiume na wa kike basi katika ripoti ifuatao Geoffrey Onditi wa Radio washirika wa Shirika la Utangazaji Kenya KBC amezungumza na baadhi ya wananchi na wanahabari wa miaka mingi katika KBC ili kupata uelewa wa nafasi ya wanahabari wanawake kwa sasa

(SAUTI)