Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyombo vya habari vyatakiwa kutoa fursa kwa wanawake

Vyombo vya habari vyatakiwa kutoa fursa kwa wanawake

Kaimu mkuu wa radio ya Umoja wa Mataifa na mratibu wa maadhimisho ya siku ya radio katika Umoja huo Flora Nducha amesema wakati umefika kwa vyombo vya habari hususani radio na mamlaka nyingine mathalani serikali, kutoa fursa kwa wanawake ambao amesema lazima wadhihirishe uwezo wao.

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa hii kuhusu siku ya radio duniani Bi Nducha ambaye ni mwafrika wa kwanza mwanamke kushika nafasi ya mkuu wa radio ya Umoja wa Mataifa amesema jamii inapaswa kukubali kuwa wanawake wanaweza.

(FLORA CLIP)