Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafasi ya wanawake katika radio bado ni finyu:Edda Sanga

Nafasi ya wanawake katika radio bado ni finyu:Edda Sanga

Licha ya juhudi nyingi za wanahabari na taasisi za habari kuwainua wanawake na wasichana katika vyombo vya habari mathalani radio bado juhudi zinakabiliana na changamoto kadhaa licha ya kuzaa matunda kwa sehemu.

Katika mahojiano maalum na Goerge Njogopa wa idhaa hii mtangazaji mkongwe nchini Tanzania Eda Sanga ambaye ni miongoni mwa wanawake wachache waliosikika mwanzoni na kutamba kupitia iliyokuwa Radio Tanzania Dar es salaam sasa TBC Taifa na ambaye kwa sasa ni Meneja wa vyombo vya habari vilivyo chini ya chuo kikuu cha DSM, anasema licha ya mafanikio hayo bado hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa kwani ikilinganishwa na wanaume bado nafasi ya wanawake katika radio ni finyu.

Kwanza Bi Sanga anaanza kwa kueleza juhudi zilizopigwa katika kuwainuwa wanawake.

(SAUTI MAHOJIANO)