Vifaa vya mawasiliano na habari vyaendelea kushika kasi duniani: UNCTAD

12 Februari 2014

Kiwango cha uingizaji wa bidhaa za habari na mawasilino yaani ICT katika msimu wa mwaka 2012, kinaripotiwa kufikia wastani wa dola za Marekani trilioni 2, ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na kiwango cha mwaka 2011 kilichofikia trilioni 1.8. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la UNCTAD. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kiwango hicho kinamanisha kwamba bidhaakamasimu za mkononi ikiwemo zile za kisasa zaidi, kompyuta za mpakato yaani laptops, na vifaa vingine moja ya vitu vilivyokuwa na mzunguko mkubwa wa kibiashara duniani.

UNCTAD inasema bidhaa hizo zimepata mafanikio makubwa na kuzidi bidhaakamazile zitokanazo na kilimo.

Kulingana na takwimu mpya zilizotolewa nchi zinazoendelea ndizo zilizojitokeza kununua zaidi bidhaa za ICT zikiwa zimepokea kwa wastani wa asilimia 54 ikilinganishwa na maeneo mengine.

Ripoti ya  UNCTAD ambayo katika utafiti wake wa mwaka 2012 iliongeza baadhi ya maeneo ya huduma, inasema kuwa soko la ICT linaonekana kuwa kigezo mbadala ya kukua kwa hali ya uchumi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud